ads
Showing posts with label Alikiba. Show all posts
Showing posts with label Alikiba. Show all posts

Wednesday, 21 December 2016

ALIKIBA KAFANYA KILE WASICHOKIAMINI

Na.Mtu Makini
Mara nyingi sisi binadamu tumekuwa hatuamini katika kinachoitwa "Second Chance"
..Wengi tumekuwa tukiamini kwamba jambo likipita na mtu ukashindwa basi hakuna namna nyingine ya kulifanya likawezekana! Wengi tumekuwa na misemo kama "yule muda wake ushapita" "huyu alikuwa zamani" kwa sasa hawezi kufanya kitu! Hii imekuwa ikikatisha tamaa watu wengi na kuhisi kwamba hawawezi sahihisha makosa ya zamani, na pengine hawawezi kufanya zaidi ya wanavyofanya walivyofanya!

Msanii wa Bongo fleva ajulikanae kama Alikiba baada ya kukaa kimya katika muziki kelele nyingi zilipigwa za kumtaka arudi, naye bila hiyana aliitikia wito wa mashabiki na July 24 ya mwaka 2014 aliachia single mbili "Mwana" na "Kimasomaso"!
Single ya Mwana ilipokelewa vizuri kila kona ya na nje ya mipaka, huu ukawa mwanzo mpya wa safari ya kimuziki ya AK...wengi walimtia moyo na yeye akasonga mbele! Hapa kelele zikaanza kusikika kwamba AK alikuwa zamani, kwa sasa AK si chochote na AK alikuwa yule wa Cinderella..na hawezi kufika popote kwani muda wake umeshapita, hapa kuliibuka watabiri wa kila aina wakitabiri kusgindwa kwa AK!
Haikupita muda video ya Wimbo wa Mwana ilitoka, huku ikiwa ni video bora kabisa kwake kuwahi fanya toka aanze muziki..hapa kundi la watu likaibuka na kudai video ni mbaya sana, amebugi na haitafika kokote..tabiri zikaendelea ila video ikachezwa ndani ya Tanzania, Afrika na mpaka vituo vya Tv vya Ulaya huku mpaka sasa video ya Mwana ikiwa na viewers 9m+ youtube!
Mwaka huo huo wa 2014 wimbo wa mwana Ulimwezesha kupata tuzo 6 katika tuzo za KTMA...huku collabo yake na Mwanafa "kiboko yangu" ikipata tuzo ya collaboration bora kwa mwaka huo! Mayowe yakaendelea kupigwa kwamva AK hakustahili zile tuzo!!
Baada ya hapo akatoa single nyingine "chekecha cheketua" wimbo ambao ulihita ndani ya masaa 24, ni wimbo ambao ulivunja rekodi ya mkito katika kupakulia na kusababisha mtandao kuzidiwa, lakini bado watu hawakulipenda hili..tena wengine ni miongoni mwa waliomtia moyo wakati anaianza safari, tabiri zikaendelea kwamba hakuna lolote atakalofanya baada ya hapo, wapo walioanza kusifia wimbo wa mwana na kupinda Chekecha cheketua. Baada ya video kutoka maneno yakawa yale yale kama ya video ya mwana!

Baada ya hapo ilisikika Lupela ambayo nayo ilipondwa sana, si video wala si audio..hapa watabiri wa mambo wakawa wanajaribu kuhitimisha tabiri zao!
Baada ya Lupela ilikuja kutoka "Aje" hii ni kama ilikuja kukata ngebe za walio wengi, wale wakosoaji walishindwa nini cha kukosoa kuanzia audio mpaka video...Aje ikawa si wimbo tu ila ni zaidi ya wimbo, sasa ni takribani miezi 6 toka wimbo huu utoke ila uweza kumpa Alikiba tuzo 11 zikiwemo "Best African Act za MTV pia African Oscars..AK ameendelea kupata nomination lukuki kuanzia mitandaoni mpaka katika tuzo za vituo vya redio na TV...

Ni ndani ya mwaka huu AK alisainiwa katika lebo kubwa kabisa duniani "Sonny music" huku pia akipata ubalozi wa Wildaid!!


Ni mwaka 2016 ambao AK kafanya collabo nyingi zaidi na kuwatambulisha katika game hata ambao walikuwa wamesahaulika! Zile kelele kwamba hatofika popote ihali bado zinaendelea yeye kila siku amekuwa akiwaza kwenda mbele
Kwa uchache huu mwaka kafanya collabo hizi ambazo zote zimefanya vizuri na zinaendelea kufanya vizuri..
1. Unconditionally Bae_Saut Sol
2. Jike shupa_Nuhu Mziwanda
3. Mboga Saba_Mr Blue
4. Nisamehe_Baraka da prince
5. Averina_Abby Skills
6. Kajiandae_Ommy Dimpoz
7. Nitulize_Brown Mauzo
Hivyo basi naweza kusema 2016 ni mwaka ambao umempa mafanikio makubwa AK tofauti na matarajio ya wengi!
Na mwaka unaokuja naamini kuna mengi zaidi toka kwa AK, watabiri wa mambo nafikiri huu ni wakati wa kufuta zile tabiri zenu maana nina imani zitaendelea kuwaumiza kila kukicha!!

Sunday, 11 September 2016

Sony ya Davido na tahadhari kwa Alikiba























Na.Mwanakalamu
Ni miezi kadhaa tangu mwanamuziki wa bongo Alikiba aingie mkataba na kampuni inayohusika na usimamizi wa wanamuziki duniani.Sony ikamfanya Alikiba kuwa mwanamuziki wa pili kwa upande wa Afrika kupata kile kiitwacho 'global deal' chini ya sony Afrika.
Mengi yaliwatoka wapenzi na mashabiki wa muziki pande zote Afrika hasa Tanzania.Kuna waliompongeza na kuna walioonesha walakini pia kuna wale waliomkejeli kila mtu akiwa na sababu zake.Wale waliompongeza wakaja na hoja kuwa kwa kuitumia kampuni hiyo kubwa duniani Ally ataweza kupanua soko la muziki wake duniani kutokana na ukubwa wa kampuni hiyo na moja ya vitu vilivyowaaminisha jambo hilo likikuwa ni kuwa nyimbo za Ally zingeweza kuuzwa na kutangazwa kwote duniani.Pia walidai kuwa itakuwa njia rahisi kwa Alikiba kuwashirikisha wanamuziki wengine walio chini ya Sony kwote duniani hivyo kutanua wigo wa muziki wake.
Waliokuwa na walakini walikuwa na hoja kubwa kuwa menejimentinza nje ya Afrika zimekuwa zikishindwa sana kuendana na mfumo wa muziki wa Afrika hivyo ni hatari sana kwa muziki wa Ally kwani angeweza hata kupewa likizo ndefu ya kutoa nyimbo ama kushindwa kuingia baadhi ya mikataba hivyo kumfanya asiwe huru.Ingawa hoja hii ilikuwa inapingwa na wengine kuwa licha ya kuwa kampuni hiyo ya nje ya Afrika lakini tawi hilo ni la Afrika hivyo lazima watakuwa wanefanya utafiti wa soko na utamaduni wa muziki wa Afrika kabla ya kuwekeza ili kupata faida.Si hivyo tuu walienda mbali kudai kuwa Ally alionekana kuzoea menejimenti zenye mlengo huo kwani amekuwa chini ya Rockstar 4000 yenye uhusiano na Sonny kwa muda sasa na amepitia hizo likizo na amekuwa bora zaidi ya alivyokuwa huko nyuma ikumbukwe kwa tunaofuatilia muziki wa Bongo Ally hakuwahi kuwa namba moja hata walau mbili kwenye muziki wa Bongo ila leo hii kila mtu anajua alipo na amefika hapo akiwa chini ya usimamizi wa kampuni yenye asili ya nje ya Afrika ambayo wengi wanailaumj kwa kuwapoteza wanamuziki wa Afrika rejea Redsun.
Wale waliokuwa wakikejeli walikosa hoja lakini wengi walitaka kuwajibu wale waliokuwa wakishabikia kwa kuwacheka kwa mafanikio hayo ya Ally.Hawa wanabaki katika obwe la fikra ama katika fikra mfu kwani kila akifanyacho ama kimhusicho Ally ni kibaya na tatizo kwako.
Juzi Davido ambaye yupo chini ya Sony aliimaliza siku kwa kujilaumu kwa kosa la kuingia Sony akijilaumu kwa kuingia nao mkataba kwani ni mwezi wa tisa sasa hajatoa wimbo.Alikaribia kutoa wimbo lakini ghafla mambo yakakwama.Wahenga walisema mwenzako akinyolewa tia maji basi watu wakataka kuti maji kujiandaa kunyolewa  baada ya Davido kunyolewa.Wengi ni mashabiki wa muziki wa Ally wakiwa na hofu kuwa muziki wa Ally pia unaelekea kuzikwa kama vile wa Davido unavyolazimishwa kuzikwa ukiwa hai kabisa.Wengine ni wale wa kutoa kebehi wakija na hoja za kuwa Davido kaanza Ally atafuata lakini hawa nao wanaweza kupuuzwa kwani leo wanaona muziki wa Ally unazikwa wakati walishauaminisha umma kuwa muziki wa Ally ulishakufa na kaburi lake limeshapoteza hata alama.
Kuna kitu hapa tunatakiwa tujiulize kama tatizo ni Sony ama wanamuziki wa Afrika?Je,mikataba  wa Davido na Sony na Alikiba na Sony inalingana kipengele kwa kipengele?Si tuliambiwa Davido alilipwa pesa kama alivyolipwa Adele ingawa kwa Adele alipewa bilioni nyingi huku Ally akiambulia kupewa ahadi za kuutanza na kuunza muziki wake huku na huko duniani na kila kitu kinaonekana?
Je, wanamuziki wa Afrika hawana ubavu wa kuyashitaki makampuni ya nje yanapokiuka mikataba?
Au wanamuziki wa Afrika ndio tatizo, wakiendelea mazoea na usela kuliko kufuata mikataba?
Au mbwembwe tuu za kuoneshwa dunia nzima kuwa wameingia 'global deals' huwafanya wasivione hivyo vipengele vya likizo ndefu ambazo huja kuwasumbua?
Ama wanamuziki wa Afrika huangalia tuu upepo nani katoa wimbo naye akamfunike kitu ambacho wameshindwa kushawishi viwepo kwenye mikataba yao?
Tukiyajua majibu ya maswali hayo ndipo tuanze kuwalaumu Sony na menejimenti nyingine za nje ya Afrika vinginevyo tuwaache wanamuziki maana wanamajibu ya maswali hayo.
Naomba kuwasilisha.

Thursday, 21 April 2016

ANAITWA ALLY SALEH KIBA





Na.Mwanakalamu

Alikiba ama King kiba alianza harakati za muziki kitambo kidogo tofauti na wanamuziki wengi wanaotamba kwa muda huu.Mwanamuziki huyu anayetamba na nyimbo kadhaa mjini akiwa chini ya usimamizi wa Rockstar 4000 hajaanza leo kutoa hit baada ya hit na tangu 2006 alionekana kuteka masikio na akili za watu wengi na mwaka uliofuata alikuja na albam iliyokuja kuvunja na kujiwekea rekodi ya mauzo.Ingawa mitandao ya kijamii haikuwa na nguvu sana katika kutangaza nyimbo na kazi za wanamuziki mwanamuziki huyu alifanikiwa kuwateka wengi kuwa na albam  yake iliyokuwa na nyimbo kali ambazo hazikuhitaji watu kusubiri zaidi kumkubali mwanamuziki huyu.