ads

Sunday, 11 September 2016

Sony ya Davido na tahadhari kwa Alikiba























Na.Mwanakalamu
Ni miezi kadhaa tangu mwanamuziki wa bongo Alikiba aingie mkataba na kampuni inayohusika na usimamizi wa wanamuziki duniani.Sony ikamfanya Alikiba kuwa mwanamuziki wa pili kwa upande wa Afrika kupata kile kiitwacho 'global deal' chini ya sony Afrika.
Mengi yaliwatoka wapenzi na mashabiki wa muziki pande zote Afrika hasa Tanzania.Kuna waliompongeza na kuna walioonesha walakini pia kuna wale waliomkejeli kila mtu akiwa na sababu zake.Wale waliompongeza wakaja na hoja kuwa kwa kuitumia kampuni hiyo kubwa duniani Ally ataweza kupanua soko la muziki wake duniani kutokana na ukubwa wa kampuni hiyo na moja ya vitu vilivyowaaminisha jambo hilo likikuwa ni kuwa nyimbo za Ally zingeweza kuuzwa na kutangazwa kwote duniani.Pia walidai kuwa itakuwa njia rahisi kwa Alikiba kuwashirikisha wanamuziki wengine walio chini ya Sony kwote duniani hivyo kutanua wigo wa muziki wake.
Waliokuwa na walakini walikuwa na hoja kubwa kuwa menejimentinza nje ya Afrika zimekuwa zikishindwa sana kuendana na mfumo wa muziki wa Afrika hivyo ni hatari sana kwa muziki wa Ally kwani angeweza hata kupewa likizo ndefu ya kutoa nyimbo ama kushindwa kuingia baadhi ya mikataba hivyo kumfanya asiwe huru.Ingawa hoja hii ilikuwa inapingwa na wengine kuwa licha ya kuwa kampuni hiyo ya nje ya Afrika lakini tawi hilo ni la Afrika hivyo lazima watakuwa wanefanya utafiti wa soko na utamaduni wa muziki wa Afrika kabla ya kuwekeza ili kupata faida.Si hivyo tuu walienda mbali kudai kuwa Ally alionekana kuzoea menejimenti zenye mlengo huo kwani amekuwa chini ya Rockstar 4000 yenye uhusiano na Sonny kwa muda sasa na amepitia hizo likizo na amekuwa bora zaidi ya alivyokuwa huko nyuma ikumbukwe kwa tunaofuatilia muziki wa Bongo Ally hakuwahi kuwa namba moja hata walau mbili kwenye muziki wa Bongo ila leo hii kila mtu anajua alipo na amefika hapo akiwa chini ya usimamizi wa kampuni yenye asili ya nje ya Afrika ambayo wengi wanailaumj kwa kuwapoteza wanamuziki wa Afrika rejea Redsun.
Wale waliokuwa wakikejeli walikosa hoja lakini wengi walitaka kuwajibu wale waliokuwa wakishabikia kwa kuwacheka kwa mafanikio hayo ya Ally.Hawa wanabaki katika obwe la fikra ama katika fikra mfu kwani kila akifanyacho ama kimhusicho Ally ni kibaya na tatizo kwako.
Juzi Davido ambaye yupo chini ya Sony aliimaliza siku kwa kujilaumu kwa kosa la kuingia Sony akijilaumu kwa kuingia nao mkataba kwani ni mwezi wa tisa sasa hajatoa wimbo.Alikaribia kutoa wimbo lakini ghafla mambo yakakwama.Wahenga walisema mwenzako akinyolewa tia maji basi watu wakataka kuti maji kujiandaa kunyolewa  baada ya Davido kunyolewa.Wengi ni mashabiki wa muziki wa Ally wakiwa na hofu kuwa muziki wa Ally pia unaelekea kuzikwa kama vile wa Davido unavyolazimishwa kuzikwa ukiwa hai kabisa.Wengine ni wale wa kutoa kebehi wakija na hoja za kuwa Davido kaanza Ally atafuata lakini hawa nao wanaweza kupuuzwa kwani leo wanaona muziki wa Ally unazikwa wakati walishauaminisha umma kuwa muziki wa Ally ulishakufa na kaburi lake limeshapoteza hata alama.
Kuna kitu hapa tunatakiwa tujiulize kama tatizo ni Sony ama wanamuziki wa Afrika?Je,mikataba  wa Davido na Sony na Alikiba na Sony inalingana kipengele kwa kipengele?Si tuliambiwa Davido alilipwa pesa kama alivyolipwa Adele ingawa kwa Adele alipewa bilioni nyingi huku Ally akiambulia kupewa ahadi za kuutanza na kuunza muziki wake huku na huko duniani na kila kitu kinaonekana?
Je, wanamuziki wa Afrika hawana ubavu wa kuyashitaki makampuni ya nje yanapokiuka mikataba?
Au wanamuziki wa Afrika ndio tatizo, wakiendelea mazoea na usela kuliko kufuata mikataba?
Au mbwembwe tuu za kuoneshwa dunia nzima kuwa wameingia 'global deals' huwafanya wasivione hivyo vipengele vya likizo ndefu ambazo huja kuwasumbua?
Ama wanamuziki wa Afrika huangalia tuu upepo nani katoa wimbo naye akamfunike kitu ambacho wameshindwa kushawishi viwepo kwenye mikataba yao?
Tukiyajua majibu ya maswali hayo ndipo tuanze kuwalaumu Sony na menejimenti nyingine za nje ya Afrika vinginevyo tuwaache wanamuziki maana wanamajibu ya maswali hayo.
Naomba kuwasilisha.

0 comments:

Post a Comment