Baada ya Mwanafalsafa na J-Moe kukutana katika kibao cha "Ingekuwa vipi" haukupita muda wakaja kukutana tena kwenye idea za nyimbo zao!!
Mwanafalsafa aliibuka na kibao alichokiita "Mabinti" huku Jmoe akija na "Kama unataka demu"Wakati Mwanafalsafa alimshirikisha Miriam SK yeye Jmoe alimshirikisha Q chief pamoja na Solo Thang Ulamaa...
Mfanano wa nyimbo
Wote waliegemea kwenye kusifia wanawake ambao walikuwa na majina na wasiokuwa na majina pia, Mwanafalsafa alionesha kuwa addi ted yaani dam dam wanawake wenye sifa tajwa... Huku upande mwingine Jmoe akihitaji demu mwenye sifa alizozianisha...
Watu maarufu waliotajwa na wote wawili
1. Mercy Galabawa
Ila ataweza kuimba vipi Rnb kama Stara
Hii ni sawa na Mercy Galabawa leo kuwa msela-Jmoe
Mwili utakaokufanya upende love kama Mercy Galabawa
Na macho yanayovuta kama ya Miriam wa Ikoa unaweza utangaze ndoa
2. Aminata Keita
Kama nitataka mwanya nafahamu wapi nitapata
Muite Aminata wa Keita.... Mwanafalsafa
Tukisema Miss Aminata Keita haina noma
IFM watakona muda wote ambao atasoma-Jmoe
3. Zay B, Jay dee & Ray C
kifua kama cha Zay B, kiuno kama cha Ray C na pozi kama za Jaydee-Mwanafalsafa
Nini Gado kama Zay B... Mrefu kama Basila... Designer Khadija mavazi akatuoneshee Kajala..
Nitaakikisha hakuna machozi kama Kama Jaydee
Sitazuia akisema anakuja kama Sister p-Jmoe
4. Happiness Magesse
Warefu warembo kama twiga mithili ya Happy Magesse
Mrefu siyo mfupi na nyama siyo mwembamba
Hewani kama Gesse kiuno kama Odemba-Solo Thang
5. Radhia wa Unique Sisters
Miondoko kama faudhia
Au ungependa kithethe mithili ya Radhia? -Mwanafalsafa
Lafudhi iwe tamu siyo kithethe ka Radhia
Hapo mimi nitadata kama Nature kwa Sonia-Solo Thang
Wote wawili walitaja kusifia watoto wa matajiri
Katika verse ya tatu Mwanafa anasema "Kuna mabinti wapo kamili kila idara
Familia bora akili zisizolala"
Huku Jmoe katika verse ya kwanza akisema "Bora nitoke makumbusho niende zangu Knyama, kwenye watoto wa geti kali baba mama tajiri"
Pia wote waliwataja akina Seven, Kibibi na Regina
NB: Huwa napata shida kuamini kama huu ulikuwa mgongano wa mawazo tu, japo wao walituaminisha hivyo!
Ila Kama unataka demu ya Jmoe ni my favorite!
Je wewe ipi ilikubamba, Mabinti au Kama unataka demu?
Steven Mwakyusa @2016
0 comments:
Post a Comment