Na.Steven Mwakyusa
Ukiitazama sura ya dunia hasa nchi
kavu utakutana na milima na mabonde, ipo milima ya aina mbalimbali
kutokana na namna ilivyofanyika mpaka kufikia hapo ilipo!! Milima ni
miinuko ambayo ina urefu kuanzia mita 600 toka usawa wa bahari!
#1 Milima iliyopo pwani ya Norway, Brazili, Australia, magharibi mwa
India na kwingineko inakadiriwa kuwa na umri wa miaka 1000 mpaka 1200
million!
#2 Kuna aina kuu tatu za
milima, milima ya volcano(volcanic mountains), milima mikunjo(fold
mountains) na milima tofali(block mountains).
#3 Mlima Everest ndiyo mlima mrefu zaidi katika uso wa dunia kwa maana ya nchi kavu ukiwa na futi 29,028.Mlima Everest unapatikana katika mpaka wa Nepal na Tibet barani Asia!
#4 Mlima Kilimanjaro ni wa 10 kwa urefu duniani ukiwa na futi 19,317.
#5 Milima imekuwa chanzo cha kufanyika mvua kwa kulazimisha upepo wenye mvuke kupanda juu na baadaye kusababisha mvua nyingi katika upande unaopakana na bahari (Windward side), huku upande wa pili ( Leeward side ukipata mvua chache au kukosa kabisa.
#6 Safu ndefu zaidi za milima katika nchi kavu ni milima ya Andes yenye urefu unaofikia 7200 km, katika safu ndefu zaidi ni zile za Mid-Antlantic ridge zenye urefu wa 11,300 km.
#7 Mpaka mwaka 2011 iliaminika kuwa mlima mrefu katika mfumo wa jua ni mlima Olympus mons katika sayari ya Mars wenye urefu wa 21.9 km.
#8 Mlima Rheasilvia unaopatikana katika Vesta Astroid una urefu wa 23km ndiyo mlima mrefu zaidi mpaka sasa katika mfumo wa jua (solar system)
#9 Pamoja na kutokea kwa mmomonyoko wa udongo (soil erosion) unaosababisha na mvua na upepo milima imekuwa ikipungua kwa kiasi kidogo sana, kuna wanasayansi wanaoamini katika kinachoitwa "Isostacy theory"

0 comments:
Post a Comment