Na.Mwanakalamu
Nilianza kumsikia
kwenye nimechokwa akiwa na Belle nine kabla ya kuanza kuporomosha ngoma
zilizokuwa kali kama Nidanganye, kerewa, na kuzikamata fikra za wapenda
burudani na hata wasiopenda burudani hadi pale alipotoa ngoma iliyotikisa
Afrika na mkali kutoka Nigeria KCEE Shikorobo ambayo kwa maelezo yake na hisia
za wachunguzi wa mambo ilionekana kumpa madili mengi.
Lakini baada ya kutoa
wimbo huo ambao wengi tuliamini ni kama wimbo ‘’uliotoboa’’ Afrika ghafla
Shetta akapotea hakuna ngoma mpya yake ama hata ya kushirikiana iliyotoka
kwake.Tukawa na subira na tukakaa mkao wa kula lakini matokeo yake kila
tulipolisikia ama kulisoma jina la Shetta tukawa tunakutana na taarifa sijui za
kukorofishana na mama Qaira ama amenunua gari jipya, naam ndo maisha lakini
kama mwanamuziki hatukusikia ngoma mpya.
Mkali huyo ambaye kila
aliposhirikishwa alionekana kuwafunika anaoshirikiana naye isipokuwa alipokuwa
akisimama na Diamond lazima ukubali ile tunayoiitwa ‘’Chemistry ya muziki’’
kwani ni vigumu kujua nani kamfunika mwezake ameamua kuwa kimya na kutuacha
wapenzi na wasiowapenzi wa muziki wake tukiwa hatuna cha kuongea.
Kuna wale ambao daima
tunampinga tulijipanga kumkosoa na kumwambia ameshindwa kuufunika wimbo wake wa
shikorobo licha ya kuwa alipoutoa tuliukandia na kumwambia umejaa unaijeria na
haukuwa na jipya katika bongo fleva.Lakini pia kukaa kwake kimya sisi wa upande
huo tunamwona ni kama anaogopa mafanikio ya Shikorobo hivyo ameamua kukaa kimya
ama ameishiwa kabisa.
Pia kuna kundi la pili
ambalo sisi huwa tunaamini kuwa anapanga kuja kivingine na akija atawapumzisha
baadhi ya wanamuziki kwa moto wake mkali akiwa na ‘’project’’ za maana za ndani na nje ya Afrika mashariki, sisi
daima humsubiri na kutarajia makubwa siku zote hata pale asipotuahidi.Sisi
tunajiita ‘’Wafuasi wa shetta ama team Shetta’’
kama Alikiba alikaa miaka miwili na nusu kasha akakubalika atakuwa
Shetta ambaye kwenye Kariakoo ya Abby skills alimfunika hata Kiba na kisauti
chake.
Sisi wa kundi la mwisho
wala hatumfuatilii atoe wimbo asitoe hatuna habari naye na siku akitoa wimbo
mkali tutausikiliza na kuushabikia akitoa mbaya tutaachana naye na kusikiliza ngoma kali, kwa
kifupi sie tunashabikia ngoma kali mbaya hatuna muda nazo.
Pamoja na yote hapo juu
bado tunajiuliza yupo wapi Shetta ama Shikorobo ishamlipa?
Pengine bado anaendelea
na ratiba yake ya kutoa wimbo mmoja kila mwaka ?
Atuambie, tujue.
0 comments:
Post a Comment