Na.Mwanakalamu
Unamsikia Diamond Plutnumz? ni tajiri sijui milionea sijui bilionea lakini ni tajiri, unamfahamu Mbwana Samatta yule aliyekuwa mfungaji bora wa Afrika naye ni tajiri wa kutupwa lakini nadhani wamfahamu Joti yule wa Ze komedi naye ni tajiri na maarufu pia.
Hao wote niliowataja ni baadhi ya watu waliofanikiwa kwa kutumia juhudi na vipaji vyao , swali linakuja;
Je, ni wao pekee wenye vipaji?
Bila kumung'unya maneno kuna wengi sana wenye vipaji tena vya hali ya juu , mara ngapi kijijini ama mtaani kwako unamwona mtu anacheza mpira kwa kiwango cha juu tena kwenye viwanja vibovu mipira ya ovyo chini ya usimamizi wake (yaani bila kocha)?
Mara nagpi unawaona watu wakiwa na vipaji vya kuchora tena bila hata kufundishwa wanachora picha za kuuzwa ndani na nje lakini wanaiishia kuchora vibao vya shule za msingi na sekondari kwa malipo kiduchu tena bila kutambuliwa. Kwenye kuchora nina ushahidi kuna mtu anaitwa Yohana Yohana Haule huyu ndugu ni hatari anachora kweli lakini muulize anajivunia kuwa mchoraji? utakuwa unamuumiza tuu kwani hakuna cha maana cha kujivunia kwa kipaji chake.
Kuna waimbaji wangapi mtaani kwenu ama wachezaji muziki wangapi wa kariba za kina Moze yobo anayelamba pesa za Almas kwa miaka sasa? Wapo wengi lakini wataonekanaje, hakuna namna inapelekea Diamond leo akitaka mrithi wa Yobo atavuka na kwende Nairobi ama Kinshasha kwani huyo mkali wenu atabaki kucheza mtaani ama kuonekana muhuni tuu.
Kuna watu wangapi umewaona ni mafundi kompyuta ,simu, pikipiki, televisheni , redio na magari tena bila kupitia shule ? umewahi kujiuliza watu hao wangeliona darasa je? si wangekuwa wanashindana Maabara wakihangaika kuvumbua teknolojia ya kuifanya nchi yetu kuwa ya kisayansi?
Hakuna kitu.
Sitaki kukumbusha wale rafiki zako mabingwa wa mpira wa kikapu, wavu na mabingwa wa riadha na kuogelea kwani utasikitika tuu wameishia kuwa walevi na mama walizeeka baada ya kufeli darasani huku vipaji vyao vikiwa si bidhaa ya kumfanya tajiri kama Diamond.
Wala sitaki kuwakumbusha wale wachekeshaji waliokuwa wakiwachekesha darasani leo wapo tuu nyumbani hawana hata hela ya chumvi wanamwangalia joti kwenye televisheni za majirani zao ama kwenye mabango barabarani.
Sitaki kabisa kukumbusha wale ndugu zetu waliokuwa wakiigiza sauti za walimu ama hata za walevi barabarani na kutufanya tusiamini kama kweli inawezekana kufanya hivyo.
Unataka nikuulize Moringe ana utajiri ama umaaruufu nje ya facebook licha ya kuwa na uwezo wa kuandika kitu ambacho kitakufanya ujiulize aliwaza nini kabla ya kuandika.
Hii ndiyo Afrika ambayo elimu ni yale ya
kwenye mtaala pekee na kufeli mtihani wa darasani basi ni umbumbumbu ,
ingawa inawezekana kabisa kipaji kikawa mtaji.
TUFANYE NINI.
Natamani kuona tukifanya kitu kwa kizazi tulichopo, nakuomba rafiki yangu niadikie mtu unayeamini ana kipaji kama yupo facebook itapendeza andika jina na kipaji(uwezo) wake kisha tuwaunganishe watu wa makundi hayo waunde umoja na kujadili namna bora ya kuvitumia vipaji vyao.
Mfano wachoraji wajuane hapa na kuunda umoja wao ambao utawafanya wajue namna ya 'kutoka' na wale waliofanikiwa wawaeleze wenzao jinsi ya kunufaika na vipaji vyao wale wachekeshaji pia, waandishi, mafundi na wengineo hivyo hivyo.
TUFANYE HIVYO KWA FAIDA YETU NA TAIFA.
Natamani kuona tukifanya kitu kwa kizazi tulichopo, nakuomba rafiki yangu niadikie mtu unayeamini ana kipaji kama yupo facebook itapendeza andika jina na kipaji(uwezo) wake kisha tuwaunganishe watu wa makundi hayo waunde umoja na kujadili namna bora ya kuvitumia vipaji vyao.
Mfano wachoraji wajuane hapa na kuunda umoja wao ambao utawafanya wajue namna ya 'kutoka' na wale waliofanikiwa wawaeleze wenzao jinsi ya kunufaika na vipaji vyao wale wachekeshaji pia, waandishi, mafundi na wengineo hivyo hivyo.
TUFANYE HIVYO KWA FAIDA YETU NA TAIFA.
Share ujumbe ufike mbali.
0 comments:
Post a Comment