Ilikuwa majira ya asubuhi, Jumanne ya tarehe 11 mwezi septemba mwaka 2001 ambapo dunia ilipatwa na mshtuko kutokana na mashambulizi ya kigaidi ndani ya ardhi ya Marekani!
Yalikuwa ni mashambulizi ya aina yake kwa namna yalivyoratibiwa na kutumia ndege kama silaha!! Magaidi walifanikiwa kujipenyeza ndani ya ndege kama abiria wa kawaida na baadaye kufanikisha utekaji na kufanya mashambulio!!
Ndege mbili zilitekwa na kushambulia majengo pacha ya kituo cha biashara cha kimataifa (WTC)! Ndege zilizohusika ni American Airlines Flight 11 na United Airlines!
Ndege nyingine American Airlines flight 75 ilishambulia yalipo makao makuu ya jeshi la Marekani(Pentagon) huko Arlington County katika jimbo la Virginia!
Ndege ya nne ilitekwa na kuelekezwa kwenda katika mji wa Washington DC ... na inasemekana target ilikuwa ni kushambulia ikulu ya Marekani, ndege haikufanikiwa kufika WDC na ikaanguka katika jimbo la Pennsylvania!! Duru za awali zilidai kuwa abiria walijaribu kupambana na magaidi hali iliyopelekea hiyo ndege kuanguka, hii ilikuwa ni United Airlines Flight 93!!
Takribani watu 3000 waliuwawa huku wengine zaidi ya 6000 wakijeruhiwa... Mashambulio haya yalisababisha hasara ya jumla $3 trillion!!
Baada ya tukio la Sept 11 lawama na shutuma mashambulizi ziliangushiwa kwa kundi la Al-Qaeda!! Osama Bin Laden kiongozi mkuu wa kundi hilo alikana kuhusika kwa namna yeyote ila aliwapongeza wale waliotekeleza hayo mashambulio!!
Haukupita muda serikali ya Washington chini ya Rais George Bush iliitaka serikali ya Afghanstan ambayo ilikuwa chini ya utawala wa Taliban imkabidhi Bw. Osama mikononi mwa serikali ya Marekani mbali na hapo ingekabiriwa na mashambulio ya kivita!! Siku ziliyoyoma, serikali ya Taliban chini ya Mullar Omar iligoma kumkabidhi Osama, mashambulio ya anga na hatimaye ya ardhini yalifanyika na kuufutilia mbali utawala wa Taliban!! Northen Alliance waliokuwa waasi kwa wakati huo walifanikiwa kudhibiti mji wa kabul wakisaidiwa na jeshi la Marekani!!
Licha ya mashambulio makali hasa katika milima ya Torabola ilikodaiwa kuwa ndiko yalikuwa makazi ya magaidi katika mahandaki, si Osama wala Mullah Omari aliyepatikana!!
--------*------
Sasa takribani miaka 15 imepita toka mashambulio haya, wapo wanaoamini kwamba Us haikushambuliwa bali lilikuwa tukio la kutengenezwa tu ili kukamisha mission zao! Hizi zinaitwa conspiracy theories, ambazo mara nyingi huwa zinaacha maswali mengi yasiyo na majibu!
0 comments:
Post a Comment