ads

Friday, 16 September 2016

Kutoka Komando Jide hadi Ruby


Kuna wakati ubora wa msanii unaweza ukapimwa kwa idadi ya collabo anazopata!!  Msanii anapokuwa katika mafanikio basi wasanii kuanzia wanaoitwa underground mpaka wale wakubwa watatamani kufanya naye kazi!!

Hili pia limekuwa kielelezo cha mafanikio wa wasanii wa kike kwa hapa nyumbani!  Wengi wamekuwa wakishirikishwa katika nyimbo za wasanii wakubwa na wadogo hasa katika viitikio,  huku wakitaraji kuvuma kupitia majina ya wasanii husika!!

Kama ilivyo ada kila zama huwa na kitabu chake,  hivyo wasanii wa kike wamekuwa wakipokezana katika kugombewa kushirikishwa!

~Lady Jay dee ; Miaka ya mwanzoni ya 2000 kila msanii alitamani kufanya kazi na Lady Jaydee,  Jaydee alifanya collabo na wasanii lukuki kuanzia Mr II(Mambo ya fedha na Muda mrefu),  Mangwea(Sikiliza),  MwanaFa(Alikufa kwa ngoma,  Msiache kuongea na Hawajui),  AY(Machoni kama watu),  Mandojo na Domokaya (Wanoknok), Mike T (Hali halisi),  Prof J (Bongo Dar es Salaan)

~Stara Thomas: Wengi walimfahamu Stara T na kibao chake cha Mimi na Wewe na baadaye Wasi wasi wa mapenzi,  kama ilivyo ada naye alipata kushirikishwa na wasanii kama Mr II(Sugu na Kiburi), MwanaFa (Ungeniambia),  baadaye pia alifanya kazi na AT,  Linex pia Alikiba na Chidy Benz.


~Ray C: Akiwa anajitambulisha katika Bongo Flava na vibao matata kama Na wewe milele,  Uko wapi,  mahaba ya dhati,  Mapenzi yangu na Sogea sogea.,  alivuta wasanii  wengi kutamani kufanya naye kazi,  moja ya kazi maarufu alizofanya ni pamoja na Ingewezekana(Dknob), Nipe Mimi (Temba), Safi hiyo(AY), Watanionaje(Barnaba),  Mama Ntilie(At na Gerry), Kama vipi (Mez B), Niko Bar(Soggy)!  Zama za Ray C zilienda zikapita,  kiuno bila mfupa ikawa story!!


~Linah: Huyu baada ya kufanya vizuri na kazi kama Atatamani na Bora nikimbie alianza kuwa kimbilio la collabo kwa wasanii wa juu na wa chini,  Linah alifanya collabo kama Yalait(MwanaFa),  Kinomanoma (Chege na temba), Wangu(Amini),  Sitaki kuumizwa (Sajna),  Yatakwisha (Benpol), Mateso (Countryboy) na wasanii wengine wachanga!!



~ Maunda Zorro-Wakati Linah akiendelea kuvuta wasanii wengi katika collabo,  aliibuka Maunda Zorro ambaye vibao vyake vya Mapenzi ya wawili na Ni nawe vilivuta attention ya wasanii wengi kutaka kuimba naye!!  Wasanii waliobahatika kuimba na Maunda ni pamoja na Steve RnB (Usinihukumu),  K-One (Yule), Feruz(Mr Police Man), Squezer(My love) na TID(gere)!  Muda ulipita naye Maunda akapita mbaya zaidi na muziki wake ukapita!!

~Ruby-Huyu ndiye ambaye kwa sasa wasanii wengi wanatamani kufanya naye kazi wakiamini wanaweza kufika mahali!  Akiwa tayari mkononi ana kazi kama Na yule,  Sijutii na Forever,  Ruby amefanikiwa kufanya kazi kama Nivumilie (Barakah the prince), Ayaya(Abdu Kiba)!  Pia kumekuwa na malalamiko ya baadhi ya wasanii kukataliwa collabo na Ruby,  na mmojawapo aliyepaza sauti ni Timbulo!  Ni Ruby pia aliyekataa kushiriki matamasha ya fiesta kwa kile anachodai kuwepo kwa maslahi duni!!


Je Ruby atafika wapi?  Ataweza kuvunja record za waliomtangulia?  Je yeye kama yeye atafika wapi na muziki wake?  Ni suala la muda tu!!

Na Steven Mwakyusa @2016

0 comments:

Post a Comment