Na. Moringe Jonasy kwa msaada wa mtandao.
Umewahi kumsikia kiongozi mmoja wa Kijerumani
amabaye alikuwa sababau kubwa ya kutokea kwa vita kuu ya dunia?
Umewahi kusikia kuhusu mateso waliyowapata
Waisraeli zaidi ya milioni mbili kabla ya kuuawa ambayo yaliongozwa na Kiongozi
huyo wa Kijerumani?
Kwa kusikia tuu simulizi za kukatwa viungo vya
mwili ili madaktari wakijerumani wapate mafunzo kwa vitendo ama wakiwekwa
kwenye vyumba vya mateso hujawahi kusisimkwa na damu yako ikapata ubaridi licha
ya mambo hayo kutukia mambo mingi yaliyopita?
Najua
hata akitokea Hitler ama mzimu wake
lazima utamwogopa na kumpa heshima ikibidi kwa kuogopa kukutwa na yaliyowapata
Waisraheri wa miaka ile lakini kuna mwanaume mmoja ambaye tarehe na mwezi kama
wa jana mwaka 1910 alizaliwa kabla ya kukua na kuishi katika zama ambazo
alilazimika kuyashuhudia mateso ya utawala wa Kiongozi huyo aliwahi kutompigia saluti.
Hiyo ilikuwa tarehe 13 juni mwaka 1936 katika
gwaride la uzinduzi wa jeshi la wanamaji la Horst Wessel.
August Landmesser(aliyezungushiwa duara) akionekana hana habari na saluti kwa Hitler(hayupo pichani).
KUMBE ALIJIUNGA NA CHAMA ILI APATE KAZI
Unawez akuwalaumu watu ambao hujiunga na vyama Fulani
ili wapate kazi , basi uanatakiwa kumlaumu na huyu bwana ambaye alijiunga na
NAZI kwa matarajio ya kupata kazi kabla ya kufukuzwa kwenye chama baada ya
kutaka kumuoa mwanamke aliyekuwa na asili ya Israeri, Irma Eckler ambaye licha ya apta vikwazo vingi wallifanikiwa kuzaa
naye watoto wawili Ingrid na Irene ambaye mkewe alijifungua akiwa
kizuizini.
Mkewe akiwa na watoto wake Ingrid na Irene
ALIWAHI
KUJARIBU KUKIMBILIA DENMARK
Mwaka
mmoja baada ya kufukuzwa kwenye chama cha NAZI (mwaka 1937) August alijaribu
kutorokea Denmark katika harakati za kulinda penzi lake lakini walikamatwa yeye
na mpenzi wake kabla ya kufanikissha azma yao.
Kwa
kifupi maisha ya mwanaume huyu ambaye alikuwa mtoto wa pekee kwenye familia
yake yalitawaliwa na mikasa na matukio mengi ya kustaajabisha hadi pale
alipopoteza maisha akiwa vitani huko Koratia Oktoba 17 , mwaka 1944 mkewe
alifariki miaka mitano baadaye huku wanae wakichukuliwa na kulelewa kwenye
kituo cha yatima huku wakigawana majina ya wazazi wao.
Akiwa kwenye sare.
0 comments:
Post a Comment