ads

Friday, 1 January 2016

MAMBO MATANO YA KUFANYA UNAPOKUTANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI (EX)


Na.Tumsifu Kaoza
1.KUWA MUWAZI. 
Kama upo tayari kuongea na ex wako mkikutana, akuulizapo swali lolote mjibu inavyotakiwa kwa majibu mafupi yasiyo ya kubabaisha yenye ukweli mtupu. Kama ni ndiyo 'ndiyo' na kama ni hapana 'hapana' itakufanya kujenga utu wako na kukupa kujiamini.

2.USIJITONGOZESHE. 
Kama umeshaachana na mpenzi wako mpya kwa sababu ya huyo mpenzi wako wa zamani usifanye mambo ya kujitongozesha kama vile kukaa naye karibu kumchekea chekea au kumtega kwa namna yeyote ile kama ikitokea bado unampenda muache yeye akuanze na umsumbue katika kumjibu kwa sababu kama mlishaachana huna hakika lile kosa halitajirudia mkirudiana.

3.KUWA NA MAWAZO CHANYA. 
Wengi wanapokuwa pamoja na wapenzi wao waliopita hufikiria negative hujiuliza anawaza nini? Ananiona mbaya? Vipi kama anakuja kunionesha mpenzi wake mpya? Haya ni maswali machache yanayowapitia wengi vichwani mwao. Lakini kama ukiwa na mawazo chanaya unaweza kujiamini na uwezo hata wa kumface huyo mpenzi wako aliyepita kwa hiyo uwapo na ex wako fikiria mawazo chanya.

.RELAX. 
Muda mwingi watu mnapokutana na wapenzi wenu waliopita huwa mnapanic kitu ambacho unatakiwa kufanya ni kutulia na kuvuta hewa nyingi ndani na kutoa nje hii hujenga kujiamini na kuondoa hofu iliyojengeka usoni mwako.

5.USIONESHE KUKOSA FURAHA KATIKA PENZI LAKO LA SASA. 
Usimpe nafasi x wako kujiona yeye ni muhimu sana katika maisha yako yaani ajione yeye alikuwa ni furaha yako ya pekee hata kama huyu wa sasa hana tofauti na yeye lakini jitahidi kujiweka sawa na kumuonehsa kuwa hakuna tatizo huyu wa zamani ili kujenga kujiamini kwako kila mnapozungumzia habari za mahusiano.
Heri ya Mwaka Mpya.

1 comments:

  1. Nilimkuta mke wangu akinidanganya baada ya kugundua jumbe kati yake na mpenzi wake wa zamani kwenye simu yake. Nilihuzunika sana kwa sababu sikuweza kuelewa nilichofanya ili kustahili hilo. Nilipomkabili kuhusu hilo, alikasirika na kusema alitaka talaka.

    Nilimpenda sana, na sikuweza kuvumilia wazo la kumpoteza mke wangu na watoto kwa mwanaume mwingine. Kisha nikajulishwa kwa mtu aliyedai kusaidia kufufua mapenzi katika ndoa zenye matatizo.

    Saa chache baada ya Dkt. Dawn kusema amekamilisha uchawi, mke wangu alinipigia simu nilipokuwa kazini, akiniomba nimsamehe na kusema anaomba msamaha kwa kutaka kuondoka kwenye ndoa yetu.

    Nilishtuka kabisa. Machozi yalinitoka mara moja kwa sababu niliamini kweli kwamba nilikuwa nimepoteza familia ambayo nilikuwa nimejitahidi sana kuijenga.

    Ikiwa unapitia matatizo ya uhusiano na unahitaji msaada, unaweza kuwasiliana na Dkt. Dawn kupitia WhatsApp: ( +2349046229159 ). dawnacuna314@gmail.com

    kwa suluhisho la haraka na lenye nguvu.

    Huduma zinazotolewa:
    • Uchawi wa mapenzi
    • Kurejesha upendo na furaha katika mahusiano na ndoa
    • Kuvutia mpenzi mpya
    • Usomaji wa mahusiano
    • Tambiko za bahati nasibu
    • Kurejesha mali iliyoibiwa
    • Mwongozo wa hatua kwa hatua kwa masuala na changamoto za kibinafsi

    ReplyDelete