ads

Monday, 8 February 2016

HAWAHITAJI MANENO MAGUMU KURIDHIKA

Na.Moringe Jonasy
Wengi husema mwalimu wao kipofu, ndo maana haweshi kulia lia kwa matokeo ya ''ujinga'' walioufanya.Kwangu nawaona mashujaa kuliko mashujaa wote waliowahi kutokea duniani.
Hushawishika kwa maneno machache na mepesi.
Hutubeba karibu mwaka mzima.(miesi tisa)
Hawana roho mbaya , labda wawe wamehamishwa akili na mateso.(si wepesi kutenda ubaya)
Hutuleta duaniani kwa uchungu na maumivu makali.(ni uchungu unaotisha hata kusimulika)
Huuumia kuliko viumbe wengine tukiwa kwenye taabu(nakumbuka kisa cha mama kuwatafunia watoto mahindi ya kukaanga kipindi cha elnino)
Hawa ni wanawake , viumbe ambao kutwa tunasikia na kuona wanatukanwa na kupitia manyanyaso makubwa,,, mara ngapi umesikia viungo vyao vya siri vikiwa ni matusi maarufu?
Hawa ndio viumbe ambao katika kila majuma manne katika robo tatu ya maisha yao hupata maumivu makali ya tumbo.(Naamini Mungu ana kusudi lake katika hili)
Lakini licha ya yote neno pole kwao ni la maana na lina nguvu kuliko fuko la noti.Hawa ndio mabingwa wa kuwasamehe wenzi wao hata kama wamewaumiza kwa kiwango gani.Hawa ndio waliamua kulihalalisha lile neno la ''shetani alinipitia'' likawa sehemu ya msamaha na ukapokelewa.
Nani asyejua kuwa ukiwaambia nitakuoa wanaamua kutua mizigo na kukupenda kweli? si kwa sababu hawajui ugumu wa ndoa lakini wanaamini kwa kutimiza sakramenti ya ndoa(kwa wanaoamini) watakuwa wamempendeza Mungu.
Hawa ndio viumbe wanaosamehe hata wakifumania, mara ngapi tunasikia na kuona familia zina watoto wa mama tofauti , si kwama hawawezi kufanya watoto wawe na baba tofauti .Hapana wanaweza ila uaminifu na roho zao nzuri huwafanya wabaki wakivumilia na kuwalea watoto wa wanawake wenzao kisa neno la ''nilipitiwa''.
Ndiyo maana hata nikisikiliza nyimbo za mapenzi huwa nakutana na maneno mepesi sana na zikwafurahisha na kuwapoza mioyo , sikushangaa kuyaona maneno mepesi ya alikiba kwenye wimbo wake mpya wa Lupela , najua anajua watu aliowaimbia watayapenda na kuyaona ni zawadi kubwa sana na ya thamani badala ya kuburudisha nafsi wao mioyo yao hutibika kwa maneno ya faraja kama yale. Sishangai kumsikia Diamond akiwaimbia kila siku maana wanahitaji faraja ya kupooza maumivu yao ambayo wanasababishiwa na wanaowaamini na kuwapenda.
Bado naamini ni watu wenye akili sana kwenye ulimwengu huu uliojaa mabalaa wanaposamehe wakati mwingine hufanya hivyo kwa huruma na hawataki tuumie lakni wengi tumekuwa tukiwaona ni wajinga, labda kweli ni wajinga sana kwani hutunza sumu miilini mwao ambayo baadaye huwaangamiza kwa lengo la kuwaponya wanaowapenda.
Kwa wema wao wamenifanya niamini hata huyo mtoto pichani ni wa kike maana wanawake wamebeba roho ya kubeba maumivu ya wenzao.
Nawatakiwa usiku mwema , natamani kila mmoja amwambie mama yake ma ndugu yake yeyote wa kike neno zuri la kumpa faraja na kuupoza moyo wake.
Moringe 8/2/2016

0 comments:

Post a Comment