Na.Mwanakalamu
Wiki iliyopita niliandika makala juu ya utani uliopo mitandaoni na mitaani juu ya hiki kiitwacho shule za kata.Imekuwa kawaida kwa yeyeto ambaye anachukuliwa kuwa hajui jambo basi atakuwa amesoma shule za sekondari za kata.Sikatai kuwa shule hizo zina mafungufu lakini si kwa kiwango cha kila 'mbumbumbu' basi ni zao la shule hizo mtoto Getrude Clement amedhihirisha hilo kwa ushahidi.
Binti huyo ambaye familia yake si ''ya kishua'' kama wengi walivyofikiri baada ya kusikia taarifa zake juu ya kuiwakilisha vyema nchi yetu kweye mkutano wa kimataifa kuhusu Mazingira.Wengi waliamini atakuwa anasoma Shule fulani ya kishua pale Mwanza kwa kujiamini na kingereza chake safi basi huyo ni ''wakishua'' lakini tofauti na wengi walivyofikiri binti huyo ni mtoto wa baba kinyozi na mama mfanyabiashara mdogo wa nyanya na vitunguu na anasoma katika shule ya kata Mnarani jijini Mwanza.
Getrude amejiunga na klabu ya mazingira ya 'Mali hai' iliyopo shuleni hapo na kwa kupitia hiyo pia amejikuta akiwa na ujuzi wa kutosha juu ya mazingira hata alivyokuwa akiviongea havikuwa vya kukaririshwa bali ni vitu alivyokuwa akivijua nadhani ni moja ya siri ya kujiamini kwake.
Getrude anauamsha umma juu ya fikra hasi juu ya sekondari za kata si tuu kwa kuongea kiingereza safi ambacho huonekana adimu kwenye shule za aina ile lakini ameonesha kuwa kuwepo shuleni hapo si kujaza tuu namba za wanafunzi wa sekondari zitumike kama mafanikio ya chama cha siasa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu.
Lakini pia amewachongea wale wanafunzi wavivu na walimu wapuuzi ambao wametumia uwepo wao kwenye shule za kata ni kama kigezo cha kufanya vibaya kitaaluma.
Kalamu yangu tunatumia nafasi hii kumpongeza Getrude kwa mafanikio hayo nkwani yamekuwa ni njia kwako ambapo umefanikiwa kufikabungeni ulipopongezwa na kupata ufadhili wa masomo kupitia taasisi ya Naibu waziri wa afya Dr.Hamis Kigwangala.Lakini pia tutakuwa tumekosea kutowapongeza wazazi wako kwa kukulea na kukuongoza katika misingi imara iliyokufikisha hapo.
0 comments:
Post a Comment