ads

Monday, 16 February 2026

Darasa anapotupa 'darasa'


 


/Unastruggle for so long (ingawa life is harder)
Everything goes wrong (Ooh)
Hold on and be strong (harder)/
Ndivyo bwana Shariff Thabit Ramadhan alivyoufungua wimbo ambao kwa kijana mtafutaji kwenye nchi ya 'dunia ya tatu' ni kama pambio la kufungia sala yake ya asubuhi kila siku.
Darasa anaanza somo lake akikutaka utembee uone namna dunia ilivyobeba mambo mengi, kuanzia namna tunavyotamani vitu vizuri lakini tunakubali kuwa tutavipata kwa kuvitafuta siyo kuigiza maisha.
Anamwangalia baki bencha na kumweleza kuwa kwao majirani hugombana lakini kwake muuaji huuawa.
Kuna kiherehere wa dawati la mbele anashauri kuhama mtaa.
Darasa anamwambia hawezi kwa kuwa majukumu yamemzidi anaishia kushukuru tu siku ikiisha salama.
Kingine shukuru kumpata 'mtoto' ambaye yupo kumpa moyo mambo yanapokuwa magumu,( ye hajampata mla nauli😁😁)
Kuna sharobaro mmoja anajilamba midomo kabla ya kuropoka 'teacher' ulipigania uhuru tangu zama za TAA ama ulianzisha TANU?
Darasa anakumbuka kuwa alianza kuwalea nduguze katika umri ambao alipaswa kulelewa asikitika tu na kuwakumbuka wana wa mtaa ambao wameozea gerezani kwa makosa ambayo hawakuyatenda.
Anawawaza wategemezi wao ambao wamebaki hawana wa kuwalea.
Kisha kipara cha "monitor " anamkumbusha wana wa mtaa waliotangulia mbele ya haki.
Anamaliza na ;
/Yooh, But life still goes on
Mtaani hakuna dill na roho zipo mkononi
Niggas wanadie kila baada ya nusu saa
Na mademu upondo gani kitaani hawataki kuzaa/
Kengele ya mapumziko inasikika na mzeee wa overrate anaanzisha pambio maarufu la mtaa...
|Even though life is harder life is harder life
Mi sikati tamaa tamaa tamaa
Siku moja ntapataa
Sijali siku nimekosa, nimepata nimekula, nimeshinda njaa
Mi sikati tamaa tamaa tamaa
Siku moja ntapataa|
Je sikati tamaa ya Darasa ni wimbo bora wa Hip hop wa muda wote?

0 comments:

Post a Comment