Na.Nyemo Chilongani
Nakumbuka nilipokuwa mdogo, nilipenda sana kusoma hadithi za Shigongo bila kujua kwamba hata mimi pia nina kipaji cha utungaji. Nilipoanza kuandika mwaka 2004, nikajiuliza, hivi siwzi kuandika kama yeye? Na hata kama nitashindwa, siwezi japo kufuata vikorombezo fulani kwenye hadithi zake, nikasema ngoja nijaribu. Hadithi yangu ya kwanza kuandika ilikuwa PASTOR BEN AND SISTER ROSE.
Bahati nzuri, mtu wa kwanza kabisa kusoma alikuwa Odero Taiya,
form one hiyo. Alipoisoma, akaniambia Nyemo umeandika hadithi kama
Shigongo, nikashtuka sana na kusema kwamba kumbe najuajuaeeee, ngoja
nisonge.
Nikajiandikiaandikia weeee, wanafunzi waliiba sana
macounter book yangu. Kwa sababu nilitumia fedha sana kwa ajili ya
hadithi, wisho wa siku na mimi nikasema kuna watu nao watakiwa kutumia
fedha kila siku au kila wiki kwa ajili yangu, nadhani imetokea kwani mtu
anakwambia nafuatilia hadithi zako gazetini...nafurahi sana.
Baada ya kila siku kusema my role model ni Shigongo, nikaona ni lazima
na mimi nimtengeneze mtu ambaye atasema Nyemo, wewe ni role model wangu.
Ilikuwa ngumu, kumtengeneza role model kwanza ni lazima uumie sana,
upate maumivu sana, upitie mashimo, majangwa, vizuizi vingi ila mwisho
wa siku, akajitokeza rafiki mmoja Facebook, hakunificha, akaniambia tu
Nyemo story zako zinaniinspire sana, you are my role model.
Najua wengi wanatamani kuandika hadithi kama zangu, nahisi zinapendwa
kwa sababu mtiririko wake nahisi umekaa kipekee sana. Kwa sababu
aliniambia mimi ni role model wake, nikawa na hamu ya kumuona. Ni juzi
tu katia miguu Dar, kitu cha kwanza kanitafuta. Kukutana naye ilikuwa
shughuli sana, ubize mwingi ila mwisho wa siku nikampa mualiko home,
akaja, nikapiga naye stori, tukashauriana sana. Huyu ni Moringe Jonasy Mhagama hapo pichani.
Labda alifikiri Nyemo angekuwa baba fulani au mtu wa suti, alipokuja,
picha limeanza nimemfuata lodge na kaoshi, kichwani kofia, kiunoni penzi
ya jinzi, chini sendozi, akalowa
Ukitaka kujiona kwamba wewe
ni mwalimu mzuri, ni lazima darasani kwako watoke walimu, ukiona
darasani kwako hawajatoka walimu, jua ulikuwa mbovu tu.
Namkumbuka ticha wangu wa History, Noah Simon Mwasongwe,
alinifanya nitamani kuwa mwalimu wa historia, mwisho wa siku nikawa
mwandishi, ila ningekuwa mwalimu, basi ningefundisha historia. Ndiyo
hivyo bhana, kipaji kikawa zaidi ya elimu.
Jiandaeni kusoma
simulizi yangu mpya ya NISAMEHE LATIFA uone jinsi msichana wa Kihindi
alivyotengwa na familia yake kisa kapewa mimba na mtu mweusi bila kujua
kwamba ni mtoto wa aina gani angezaliwa
0 comments:
Post a Comment