Na.Moringe Jonasy
Unakumbuka shamra shamra za mwaka mpya za mwaka huu? Achana na za miaka mingine iliyopita mwaka huu ulifanyaje?
Ulichoma matairi ya magari barabarani na kulipua baruti?
Ulikaa na
ndugu zako sebuleni mkisubiri saa sita ifike mmshukuru Mungu ama mpige
sherehe za shangwe za kuuona mwaka mpya?
Ulipatana na adui yako ama ulipotoka kwenye mkesha uliuchukia mwaka uliopita na kuanza kupanga mipango ya mwaka huu?
Huenda ulifanya mengi ama moja ya hayo au hukufanya chochote zaidi ya hayo.
Nakumbuka kwangu mwana mpya wa mwaka huu nilikuwa ndio kwanza najifunza
kusherekea maana katika vitu ambavyo ninavyo ni pamoja na kusherekea.
Huwa naona kusherekea ni kama kujitoa ufahamu tuu na kuigiza kuwa huna
shida wala tatizo lolote na kuungana na watu wengine ambao nao wanaigiza
kama wewe.
Kwa nini naigiza? Kwanza naamini kuwa hakuna furaha
halisi duniani kwani unaweza pata vyote unaanza kufikiria vipi wengine
wenye shida je, itakuwaje nikifa? Basi naishia kutulia na kushindwa
kuigiza.
Mwaka mpya huu nilijaribu kuigiza na kushangilia wakati
natoka kwenye mkesha lakini nikashindwa kuendelea kuigiza nikajikuta
nazama kwenye dimbwi la mawazo bila kujua kuna boda boda aliyekuwa
akishangilia kwa namna yake akiendesha pikipiki yake kwa mwendokasi
akanipitia na kuutegua mkono wangu wa kushoto lakini kwa bahati
sikuumizwa sana na nikapona ndani ya wiki tatu na nusu.
Nilipofika
nyumbani nikajifanya kusherekea tena huku nikichana kalenda ya mwaka
uliopita nikilaumu kwa kuwa ni mwaka ambao niliteseka sana kwa kuumwa na
mateso mengine nikiibusu kalenda ya mwaka huu kwa kudai kuwa ulikuwa ni
mwaka wa furaha kwangu lakini hadi sasa mambo yameenda mrama na nusu ya
mwaka huu ni wiki chache zijazo.
Wengi tunakuwa na matumaini
makubwa mwanzo wa mwaka kama tuuitavyo mwaka mpya lakini ukweli ni
kwamba hakuna jipya tarehe moja januari mwaka mpya zaidi ya muendelezo
wa harakati zako za kimaisha.
Upya wako ni pale unapozaliwa japokuwa mwanzo huo hutanguliwa na maandalizi ya wazazi wako.
Rai yangu kwako ni kwamba nusu ya huu mwaka isikukatishe tamaa kwa
kuamini hutotimiza malengo yako ya maisha baada ya kuona huna
ulichokitimiza ama hata kukianza baada ya miezi sita.
Maisha yako hayakomi kufuata tarehe za miaka bali mipango ya Mungu juu yako kuishi.
NIANDIKIE MTAZAMO WAKO #Mwanakalamu mwenzangu
0 comments:
Post a Comment