ads

Sunday, 24 April 2016

NANI HASA ALISTAHILI UFALME WA RHYMES MWAKA 2004?


 Na.Steven Mwakyusa(Mtu Makini)
Shindano la kumsaka mfalme wa Rhymes katika bongo flava ni moja ya shindano lililopata msisimko mkubwa kwa kipindi hicho, hii inawezekana ilitokana na kukutanishwa manguli wa muziki kwa kipindi hicho hali iliyopelekea uamuzi wa nani ashinde kuwa mgumu wa walio wengi!
Shindano liliwakutanisha Jay moe(kama unataka demu), Afande Sele(Darubini kali), Prof J(), Inspector Haroun (Bye Bye), Solo Thang(Mtazamo), Madee(Kazi yake Mola), MwanaFA(Unanitega), Mandojo na Domokaya(Nikupe nini), Soggy Dogy(Kulwa na Doto) na Dully Sykes, ila Dully alijitoa siku chache kabla ya shindano!!
Shindano liliandaliwa na Global Publisher chini ya E. Shigongo na zawadi kwa mshindi wa kwanza lilikuwa gari, japo sikumbuki ni gari ya aina gani!!
Shindano lilifanyika usiku wa tarehe 27 June(siku ya ijumaa), na hatimaye Afande Sele kutawazwa kama mshindi na kuwa mfalme wa rhymes, huku ushindi wa pili ukienda kwa Inspector Haroun na ushindi wa 3 wakichukua akina Mandojo na Domokaya!
Ushindi huu ulipingwa na watu wengi kuanzia watu wa kawaida mpaka wasanii wenyewe!!
Haikupita muda Solo Thang aliandika wimbo akipinga kile kinachoitwa kupanga mshindi, namnukuu "wengine wananirubuni eti nashindania gari, kumbe washapanga wampe nani toka awali, sitarudia kosa hata zawadi waweke meli, wanipe ghorofa mbili wanikabidhi na sheli"
Solo Thang akuishia hapo, katika wimbo wa Traveller anasikika tena akisema "Mi siyo mfalme njozi mi siyo mgambo sele"
Fid Q naye katika Mwanza Mwanza aliendelea kuthibitisha kutokukubalika kwa ufalme wa Afande, namnukuu "Mfalme wa Rhymes ambaye Soggy Doggy hamtaki, anamwita Kobe hawezi mzidi mbio farasi"
Madee naye alienda mbali na kudai hajawai ona mfalme ana nywele chafu!!
Sasa ni takribani miaka 12 imepita toka Afande Sele atangazwe kuwa mfalme wa rhymes na hajapata mrithi wake, mwaka 2005 shindano halikufanyika baada ya washiriki kudai maslahi zaidi huku wengine wakipinga kunakoitwa kupangwa mshindi ambaye ilisemekana alitakiwa kuwa Fid q, ambaye alishajinadi kuwa ni mfalme atakayefuatia baada ya Selemani Msindi!!
Je Afande Sele alistahili ufalme wa Rhymes? Kama hakustahili nani alipaswa kupewa hilo taji?

0 comments:

Post a Comment