Na.Mwanakalamu.
Juzi nilikuwa nikiongea na rafiki yangu mmoja mbaye nilisoma naye nikiwa darasa la tatu,huyu sikuwahi kuonana naye tena wala kusikia habari zake lakini juzi alibahatika kupata namba yangu kupitia facebook.
Baada ya salamu na maswali mengi ,sijui umeoa ,una mtoto, unafanya kazi gani sijui nani sijui ana wake wawili mara yule jirani alifariki na mengine mengi akagusia ile post yangu kuhusu vipaji.
Nikakumbuka naye alikuwa na kipaji cha kuchekesha ,huyu alikuwa bingwa tulicheka hadi tukasahau kufanya zoezi la kusoma kiingereza tulilokuwa tukipewa na mwalimu tuliyekuwa tukimwita Oldonyo jina ambalo rafiki yangu yule alimpa ,likawa jina la mwalimu bila hata yeye kujua.
Nikamuuliza kama anahitaji namba za wachekeshaji wenzake, lakini akakataa akasema hiyo kazi niwaachie akina mpoki maana walijiongeza na akaniuliza kuhusu ukweli wa habari kuwa mpoki ni mtangazaji, nilipomthibitishia akakohoa kisha akaongea kwa kusikitika.
''Ameshajitengenezea njia , unadhani ni nani hatomuajiri hata kama serikali itasema watangazaji elimu yao ile shahada ya kwanza na yeye awe na cheti, tayari ni bidhaa''
Nikaona anaongea kwa huruma sana nikaamua kumtoa huko na kumuuliza vituko vya kugombana siku za kufunga shule , lakini hakuvifurahia aliguna tuu na kuongea mengi.
''Unajua Moringe ule mwaka si matokeo yetu yalifutwa kisa watu wawili wa MEMKWA walifanya mtihani kama wanafunzi wa kawaida wakaonekana kuwa wamerudia shule kitu ambacho si sahihi kwa darasa la saba''
''Mhhh poleni sana , samahani sikuwa na taarifa hiyo kaka si unajua niliondoka nikiwa mdogo''Nilongea nikiwa siamini nilichokisikia kwani nilijua mwenzangu atakuwa alifika hata sekondari kwani hakuwa mbaya kitaaluma.
''Basi nikashindwa cha kufanya nikenda kwa yule fundi selemara aliyekuwa akichehemea mguu mmoja sijui unamkumbuka?''
''Ndiyo si yule wa kwenye mapera?''
''Ndiyo nikaanza kumsaidia kazi huku najifunza na baadaye nikawa fundi kweli , halafu si uliniambia hujaoa basi kitanda cha kumtafutia mtoto itabidi nikuchongee bure si unakumbuka siku ile yale maandazi mawili uliyokuwa umepewa na mama yako kuyauza halafu ukanikopesha halafu sikukulipa mama yako naye kwa kukufundisha biashara alikuchapa nilikuhurumia ila si unajua maandazi yenyewe niilikuwa nampa Monika''
Nakikumubuka kisa hicho na kucheka.
''Unakumbuka kumbe ,we jamaa ulinikomoa na Monika mwenyewe kaolewa''
''Si nimesema nitakuchongea kitanda bure ama unanunua vya kichina laki nane? mama nasikia umefika hadi chuo kikuu''
''Chuo wapi umasikini tuu''Namjibu kinyonge kwani anaonekana kama anawaona watu waliofika chuo kikuu ni matajiri.
''Baada ya kumaliza mafunzo na kuwa fundi kamili nikaenda VETA kusomea nipate cheti, aisee kumbe veta wanafundisha kutengeneza hadi samani zile tunazoziona kwenye televisheni sema tuu kule nyumbani haujafika umeme''
''Kwa hiyo umeshatoboa baada ya kutoka VETA''
''Hakuna cha kutoboa wala kuziba nina ujuzi na vifaa nilivyoachiwa na yule fundi wa kule nyumbani si alihama pale kijijini''
''Dah!''Nakosa cha kuzungumza.
''Basi nawachongea watu meza ,fremu za madirisha na milango, milango,vitanda kwa hela za maji wakati mwingine hata hazitoshi kunua chumvi'
Hata tenda ya kurekebisha paa la shule tuliikosa likaja kampuni wakaja kurekebisha wakati siku za nyuma tuliitwa kama wanakijiji tuu na mwisho wa siku tuapikiwa tuu ugali tunakula na kusamehewa kwenda kufyatua tofari za shule ya kata siku mbili''
''Moringe usione hii nchi wanasema inakua kiuchumi, nyie wasomi mnaamini hivyo lakini we na usomi wako huamini kama tungepewa elimu ya kuwa na vikundi ambapo tukakopeshwa vifaa vya kisasa leo hii wangehangaika madawati hadi kulifanya suala la dharula eti wanajeshi wakatengeneze, si matusi hayo?
Kama hujabadilika ile tabia yako ya kujiongeza , najua hujabadilika juzi umeandika mengi sana mazuri kuhusu vipaji umenigusa ukanifanya niingie mtandaoni kusoma mengi tuu ya kujiongeza ufanikiwe, ile komenti yako kwenmye post ya Shigongo imeniaminisha kuwa wewe ni Moringe halisi mzee wako hakukosea kukupa hili jina''.
Unasinzia eeh, lala bhana ila naamini suala la madawati halikuwa la dharula na hata tusilalamike sana.
''Sijala'' Najibu nikiwa natafakari mengi juu ya maneno yake.
''Mbona kimya basi nipe jibu suala la madawati ni dharula?''
''Hapana''
''Je ,utanunua kitanda cha supamarket ama utaniagiza nikuletee?''
''Hata cha kwako tutaweka supermarket kaka''Namjibu kwa hamasa.
''Kweli?''
''Ndiyo''
''Nasubir''
.........simu ikakakata nikampigia akawa hapatikani.
Share ifike mbali tupate jibu kama kweli suala la madawati lilikuwa la dharula.
0 comments:
Post a Comment