ads

Thursday, 14 April 2016

OMMY DIMPOZ? SIAMINI

Na.Mwanakalamu
Jina Ommy Dimpoz likitajwa nchini kila mtu atajiwa na taswira ya mtu mmoja ambaye aliikamata Afrika mashariki kwa nyimbo zake kali ambazo zilikuwa zikienda kuikamata Afrika nzima.Mtu ambaye ndiye alitoa 'hit' baada ya 'hit' aliyetoa Nai nai , baadaye, Me and you, Tupogo, Wanjera na Ndagushima.
Utamkumbuka Ommy aliyekuwa akionekana mshindani wa Diamond Plutnumz kwenye muziki, Ommy ambaye wengi tunaamini alitufanya tukamfahamu binti mmoja ambaye leo hii ni moto wa kuotea mbali barani Afrika baada ya kumshirikisha kwenye Me and you , Vanessa Mdee.
Naam lakini wakati taswira hiyo ikikujia akilini mwako kuna taswira nyingine itajiingiza akilini mwako taswira yenye maswali mengi kuwa yupo wapi huyu mkali?
Utajijibu mwenyewe kuwa yupo bongo na huwa anaenda Nairobi na Marekani anafanya nini?
Pia utajijibu mwenyewe kuwa ni mwanamuziki ambaye ametoa wimbo uitwao Achia Body ambao video yake ni aibu kuiangalia ukiwa na wenzako hasa kama ni mwanaume , utajilazimisha kutafuta funguo mfukoni, video ambayo ina mashairi mepesi ambayo angeimba mtu kama Nuh Mziwanda basi wimbo wake ungeishia kutambulishwa kwenye stesheni za redio na televisheni na kuwekwa kapuni lakini kwa kuwa ni Ommy wengi wakhisi kuna kitu cha ziada kwenye wimbo huo na kujaribu kukitafuta na kuufanya wimbo huo kushika chati kwa muda fulani kabla ya kuzimwa taratibu.
Ni Ommy huyu huyu ambaye aliimba na J Martins ambaye leo hii hasikiki kama ni mwanamuziki , show za peke yake ama zile pamoja kubwa hazisikiki tena.
Ameamua nini ama ndo ameridhika na kuwa kama Sam wa Ukweli ama Marlow?
Anataka kupumzika kama Ally kiba?
Ameamua kufanya biashara nyingine?
Majibu anayo yeye , ila kwangu nilianza kuhisi kupotea kwa mkali huyu pale tuu alipotoa Tupogo ambapo nilijua ni nyimbo zinazotegemea zaidi nguvu ya mwanamuziki kwenye media na si ukubwa wa wimbo alipotoa ndagushima hata wanjera nikaona ni yale yale wimbo mtamu lakini hauna uwezo wa kuishi muda mrefu.
Ommy Dimpoz? Wala siamini kama ndo kaamua kupoa hivi huenda kuna mambo matamu yanakuja maana wanamuziki hawa nao wana 'timing' zao.

0 comments:

Post a Comment