Mpenzi
Nimekuzoea sana,
Nakupenda sana sana,
Kukuacha siwezi,
Nalalama?
Ndiyo nalalama sana,
Sababu sitaki ufanye ukifanyacho,
Kujitenga nami.
Makovu uliyonipa
Yawe ushahidi wa penzi,
Ushahidi wa nguvu ya msamaha,
Nautamani uzee wetu,
Uzee tukiwa pamoja.
Nimekukosea ndiyo
Umenikosea sawa,
Nikuombapo msamaha,
Naitafuta amani,
Ukoseapo natamani neno samahani,
Nisipolisikia,
Nahisi umekusudia,
Naona umependa niumie.
Nifichapo aibu zako,
Natamani ufiche na zangu,
Nakupenda wewe,
Nawapenda wanetu,
Usiponipenda,
Nakosa nguvu,
Nakosa kujiamini,
Nakosa kila kitu.
Hayupo nitayempenda,
Walau robo ya nikupendavyo,
Unanichukia?
Hunipendi?
Hunitaki?
Nakuuliza ili useme hapana,
Si ujinga ni uanaume tu.
Usiniache
Usiwape ushindi wasiotupenda,
Nakupenda mpenzi,
Sijawahi kukuchukia,
Natamani watoto wauone uzee wetu,
Tusiwe wabinafsi,
Tupendane.
Ukikosea sema samahani,
Usiseme na wewe ulikosea,
Mpenzi,
Nakupenda sana.
0 comments:
Post a Comment