ads

Wednesday, 14 December 2022

BARUA ZA MAPENZI


 











Mpenzi wa moyo wangu,

Faraja wa nafsi yangu,

Malkia wangu wa huba,

Njozi watia rutuba.


Nikuandikie nini,

Kile kilicho thamani,

Sitowaza kukuacha,

Wewe mpenzi si kocha.


Nikupe zawadi ipi,

Naomba isiwe pipi,

Ingawa unaipenda,

Thamani umeshapanda.


Njoo karibu mpenzi,

Njoo uanzishe njozi,

Njoo usiweke ufa,

Njoo nikupe nyadhfa.


Mpenzi nimefurahi,

Wewe kwangu ni sahihi,

Nipende bila uoga,

Kwako siwezi kuaga.


Uwe shina la uzao,

Niwaze kila uchao,

Kwa upendo nitakesha,

Wewe ni wa maisha.


Uje tukuta uzee,

Mpenzi unizoee,

Hadi tunajikongoja,

Kufanana siyo hoja.


Nikichoka unikande,

Kwa utani uniponde,

Siogope kunicheka,

Wala hautoachika.


Chakula chako kitamu,

Hakitoniisha hamu,

Sitothubutu kulala,

Kisema vyema sijala.


Sione haya banati,

Nikikufanya chapati,

Ukichoka nasimama,

Kishindwa nambie homa.


0 comments:

Post a Comment