ads

Tuesday 21 November 2023

SIKU ZA UJANA WA DIEGO COSTA












Na. Kenny Anjelina

Aliamua kuacha starehe zote za nchini Brazil. Diego Costa the trouble some, akaacha pombe na bata za mitaa ya Rio de Janeiro na Santos.
Akaacha warembo wa fukwe za huko Brazil ambao huzurura na bikini huku wakinywa wine.
Akaicha nchi yake ya Brazil, akaliacha soka murua la samba akanunua uraia wa nchi ya Uhispania. Wahispaniola wakampokea, wakampa jezi namba 19. Wakamuimba kwenye Euro, wakamuimba kwenye Olimpiki, wakamuimba kwenye World Cup.
Mtukutu Diego Costa alikuwa mtu bhana. Wakati akiwa na jezi ya Chelsea na Atletico De Madrid alikuchezea kwanza rafu afu anaweka kwenye kamba. Hakuwa mlaini kama Olmo wa Uhispania ya leo.
Mwaka 2014 Mtukutu Diego Costa alisafiri na timu ya taifa ya Uhispania hadi Brazil kwenye mashindano ya kombe la dunia. Na ndo huko hadithi yangu inaanza.
Uhispania, Chille, Uholanzi na Australia walipangwa kundi 1. Wabrazil wakawa wanaomba Mungu Mtukufu Diego Costa na Hispania yake watolewe kwani wangetukanwa matusi mengi kutoka kwa Costa. Waliogopa kebehi za Costa kutwaa taji kwenye ardhi ya Brazil.
Mechi ya kwanza Spain wakapigwa 5-1 mbele ya Uholanzi. Shukrani kwa Van Persie na the killer Arjen Roben. Mechi ya pili Spain akafa 2-0 mbele ya Chille ya Vidal na Alexis Sanchez.
Hadi hapo Spain wakawa wametolewa. Hadithi ikawa fupi kwa the trouble some Diego Costa.
Wakati anatoka uwanjani wabrazil wakaanza kumzomea huku wakiimba "Adias spana! Adias Amigo!" Yaani kwaheri Rafiki kwaheri mwenzetu. Wabrazil wakanywa pombe na kufurahi usiku ule.

HAPO ZAMANI ZA KALE  

0 comments:

Post a Comment